Kibira Films International ina mipango ifuatayo mbeleni:
1. Sinema ya pili ni kuhusu ukimwi. Hii sinema itazungumzia hali ya ukweli wa ugonjwa wa ukimwi katika bara la Africa. Nusu ya uandishi wa sinema hii umemalizika. Asilima kubwa (80%)ya sinema hii itakuwa kwenye Kiswahili.
2. Sinema ya tatu Bongoland...BONGOLAND II. Kampuni hii ina mipango ya kufilm sinea nzima kutoka Tanzania. Sinema hii itamfuata Juma kuangalia jinsi maisha yake yalivokuwa mara baada ya kufika Bongoland.
3. Sinema ya nne itakuwa ni juu ya uhusiano kati ya Waafrika wa kimarekani na Waafrika kutoka waishio marekani. Mpaka sasa inaonekana uhusiano ni wa kimaajabu sana na kutatanisha.
4. Sinema ya tano, itakuwa ni juu ya maisha ya Mwalimu Julius Nyerere na mchango wake katika dunia na hasahasa katika nchi ya Tanzania. Hadithi ya Mwalimu Nyerere lazima isimuliwe tena kwa vizazi vijavyo au kwa watu ambao hawakufahamu.