Maoni Ya Mkurugenzi

Huu ni mwaliko maalumu katika site hii. Hiki ni kipindi kipya sana katika sinema za kisasa. Sinema za Kiswahili. Kama unavyojua, kuna watu zaidi ya miilioni mia moja wanaoongea Kiswahili lakini mpaka sasa kuna simema chache sana zilizoandikwa kwa Kiswahili.

Sisi waswahili waishio Marekani, tuliamua kuwa lazima tufanye mipango maalumu mara moja ili kuhakikisha kuwa Kiswahili kinawekwa kwenye ramani ya dunia. Hapo ndio tuliamua na kuanza mikakati ya kubuni Bongolan.

Bongoland ni hadithi ya kijana anayeitwa Juma Pondamali. Kijana huyu alikuja majuu akitafuta hali ya maisha bora. Kama wengi wetu tunavyoaamini, maisha ya majuu ni maisha bora. Bwana Juma alikuwa na kazi yake nzuri kule Bongoland. Baada ya kumaliza shule form six, alijipatia kazi nzuri sana. Baada ya kufanya kazi kwa kama miaka mitatu, akaanza ksuka mipango ya kwenda majuu. Kwa bahati nzuri akafanikiwa na akaondoka kwenda majuu.

Kufika majuu maisha yakawa kama alivyosikia katika miezi ya kwanza. Akapata kazi, akanunua gari hata akapata na msichana wa kimarekani. Mambo yakawa safi. Baada ya muda kidogo, mambo yakaanza kubadilika. Juma akajitahidi kujaribu kumaliza matatizo hayo. Lakini matatizo yakazidi kuwa mengi.

Juma alikuwa na marafiki zake waliojaribu kumsaidia na kumwonyesha jinsi ya kuishi vizuri pale ugenini. Hapo ndipo Juma alianza kuwauliza rafiki zake swali moja la maana sana. "Je ni lipi rahisi, kuwa mtumwa aliyeshiba, au kuwa mtu mwenye njaa aliye huru". Juma aliyaona maisha ya majuu kuwa kama utumwa wa aina fulani. Akaanza kujiuliza kwa nini anaumia hivi. Hasa hasa baada ya kila mtu kumwambia kuwa maisha haya yatakuwa mazuri.

Sinema hii intafundisha kujiuliza maswali ya Juma kwa wale wenye mipango ya kwenda majuu. Je maisha ni rahisi kuumia mradi uko majuu?. Je angekuwa nyumbani angeyapata matatizo kama hayo. Juma anatusaidia kuelewa na kujaribu kujibu swali hili.

Ninakukaribisha sana kuangalia sinema hii ili ujionee mwenyewe na kujiuliza kama wewe ungekuwa Juma ungefanyaje. Je Juma anasema ukweli kuhusu majuu, je ni kweli kuwa maisha ya majuu ni kama utumwa, je Juma atafnya nini.

Uzuri wa sinema hii ni kwamba kwanza imeandikwa na waswahili, kwa hiyo wanaelewa jinsi Juma anavyofikira. Plili, ni sinema kwa ajili ya waswahili, tatu ni sinema iliyoandikwa na watu ambao wameishi maisha kama ya Juma. Wanaelewa ukweli wa mambo ulivyo.

Karibu sana na nadhani utaburudishwa na sinema hii. Kumbuka hakuna sinema za Kiswahili zilizokwisha tengenezwa kwa muda mrefu.

Tafadhali unaombwa kufika kwenye site hii mara kwa mara kujua tarehe sinema hii itakapoonyeshwa.